DHIKI YETU NI NYEPESI SANA!
“Kwa hiyo hatulegei; bali ijapokuwa utu wetu wa nje unachakaa; lakini utu wetu wa ndani unafanywa upya siku kwa siku. Maana dhiki yetu nyepesi, iliyo ya muda wa kitambo tu, yatufanyia Utukufu wa milele uzidio kuwa mwingi sana” 2 Korintho 4:16-17.
Kati ya mambo ambayo Mungu hawezi kuja kulaumiwa hata siku moja ni hili, kwamba kila kitu kinachohusu maisha yetu ya kiro na kimwili aliweka kwenye maandiko matakatifu, yaani Biblia.
Hii ndio kusema kwamba, kila swali ambalo Mwanadamu angweza kujiuliza au kumuuliza Mungu, tayari Mungu alishajibu, na hata kama tutasema kwamba hatuoni majibu yake kwenye Biblia, imeandikwa kwamba Roho Mtakatifu atatukumbusha na kutufundisha yote! Hapa inategemea ni kwa kiasi gain unashirikiana na Roho huyu wa Mungu.
Miongoni mwa amajibu mengi amabyo Mungu alijibu kabla hatujauliza ni kuhusu kile ambacho Wakristo huita MAJARIBU au MAPITO. Vyovyote utakavyoita, elewa kwamba tulishapewa majibu.
Paulo anasema, pamoja na kwamba tuna dhiki hatulegei! Ndugu zangu, dhiki yaweza kuwa chochote katika maisha yako. Lakini la muhimu kufahamu ni kwamba dhiki hizi huweza kuletwa au kusababishwa na shetani akiwa na lengo moja tu, nalo ni KUTUDHOOFISHA KIIMANI, KUTUGOMBANISHA NA MUNGU nk.
Amini usiamini, atatumia mazingira uliyonayo, atatumia rafiki, ndugu, mke, mume, wazazi, bosi wako kazini nk. Shida na changamoto kubw atuliyo nayo ni kwamba tunapoona mke au mume amegeuka na kuwa mwiba, tunakana na kumwangalia mume/mke badala ya kumuona shetani, na kasha tunageuka na kusema Mungu uko wapi?
Ndugu zangu, wapo wapendwa wanauliza Sali hili, kwa nini pamoja na kuokoka bado tupitie dhiki? Nina jibu rahisi lakini ngumu kukubalika na wengi, ni kwamba TUNAISHI DUNIANI!
Kristo Yesu kabla hajaja duniani aliishi Mbinguni, mtafute muulize kama aliwahi hata siku moja kuteswa, kudhihakiwa, kutukanwa, kupigwa mijeredi, kutemewa mate au kusulubiwa kule Mbinguni, mtafute muulize. Atakwambia kule Mbinguni hayo mambo hakuna!
Yeye Kristo aliyakuta hayo hapa duniani, ukiniuliza kwa nini nitakwambia mbali na kutimiza maandiko, pia ni kwa sababu alikuwa duniani. Tafuta Watakatifu wote kwenye Biblia, tafuta wale amabo waliishi maisha ya kumcha BWANA, tafuta wakina mama ambao walikataa kuishi kwa kutenda dhambi, watafute vijana ambao waliipa dunia hii kisogo, watakwambia waliwahi kupitia dhiki, kwa nini? Kwa sababu walikuwa duniani!
Pamoja na hayo, Paulo anasema “hatulegei; bali ijapokuwa utu wetu wa nje unachakaa; lakini utu wetu wa ndani unafanywa upya siku kwa siku. Maana dhiki yetu nyepesi, iliyo ya muda wa kitambo tu, yatufanyia Utukufu wa milele uzidio kuwa mwingi sana”
Inawezekana ni ugonjwa, inawezekana ni uchumi, inawezekana ni changamoto yoyote hapa duniani, na kwamba watu wanapotuona hatuna hela wanatucheka, wanatudhihaki, wanatukejeli, wengine hata kusema hatuna Mungu sawasawa, na utu wetu wa nje unachakaa na kupoteza kabis ataswira, hatimaye heshima yetu huw akama inashuka nk, Lakini kadri ambavyo wanazidi kukudharau na kukutweza, kadri ambavyo unapitia dhiki hiyo, UTU WAKO WA NDANI UNAZIDI KUMEREMETA, ikiwa tu unaendelea kusimama katika uaminifu mbele za Mungu!
Mbingu zinamheshimu mtu anayeshinda mapito au majaribu, Mungu anamwandalia mtu wa jinsi hii tuo.
Sikiliza, Mungu anamheshimu mtu ambaye anasema hata kama nitakosa mume/mke, SIKO TAYARI KULALA AU KUOLEWA NJE YA MPANGO NA UTARATIBU WA MUNGU! Mungu anamheshimu mtu huyu. Mungu anamheshimu mtu ambaye pamoja na kukosa kodi ya nyumba, bado anasema “SIKO TAYARI KULAGHAI AU KUIBA ili nilipe kodi!
Tena Mungu anamheshimu Mtu ambaye anasema pamoja na kukosa ada ya shule ya watoto, au ya kwangu mwenyewe bado sitamuacha YESU!
Lakini ni mpaka utambue kwamba ijapokuwa utu wetu wa nje unachakaa; lakini utu wetu wa ndani unafanywa upya siku kwa siku. Maana dhiki yetu nyepesi, iliyo ya muda wa kitambo tu, yatufanyia Utukufu wa milele uzidio kuwa mwingi sana”
|
Maneno mazuri sana haya katika kuimarisha maisha ya Mkristo na mtu mwingine yeyote yule. Nasema ni maneno mazuri kutokana na ukweli kuwa watu wengi wametetereka katika imani zao kiasi cha kukimbilia kwa shetani wakifikiri kuwa uko ndio kuna amani na uponyaji. Manthalani tunapougua na kupata shida kuu baadhi ya watu wamekuwa wakikimbilia kwa waganga wa jadi ili waaguliwe kwa kusomewa au kupigiwa ramli na kusahau kuwa dhiki ya ugonjwa ni ndogo sana kwa Mungu aliye hai katika Kristo Yesu.
ReplyDeleteUshauri wangu ni kumrudia Mungu na kumkabidhi mahitaji yetu nasi hatutoogopa lolote maishani mwetu si njaa, ugonjwa, kukosa kazi n.k
Ni kweli Tomitho, Mungu akubariki sana!
ReplyDelete